MCHENI
MUNGU NA KUZISHIKA AMRI ZAKE
UTANGULIZI
“Dunia
inaomboleza,inazimia,ulimwengu unadhoofika,unazimia,watu wakuu wa dunia
wanadhoofika.tena dunia imetiwa unajisi kwa watu wanaoikaa,kwa maana wameziasi
sheria,wameibadili amri.wamelivunja agano la milele.Ndiyo sababu laana imeila
dunia hii,na watu wanaoikaa wameonekana kuwa na hatia,ndiyo sababu watu
wanaoikaa dunia wameteketea,watu waliosalia wakawa wachache tu” ISAYA 24:4-6
Mpendwa msomaji,tafakari sana aya hizi za
utangulizi.
Unaweza kuungana na kile maandiko yanachoonyesha
kuhusu hali halisi ya Dunia yetu hii leo.
Laana inaila dunia yetu hii leo kwa sababu zifuatazo
1. “Wameziasi
sheria”
2. “Wameibadili
amri”
3. “wamelivunja
agano la milele”
Hivyo katika waraka huu, mungu anahitaji kutuonyesha
namna ya kuepukana na laana hiyo.ila tu nai mpaka pale tutakapogundua mambo
yafuatayo:-
1. Amri
hizo za mungu ni zipi?na ni ngapi?
2. Amri
hizo za mungu ni za muhimu mpaka sasa?(kizazi hiki)
3. Amri
hizo za mungu,kila mtu anapaswa kuzijua na kuzitii? Na anwajibishwa kwa kutozifahamu
au kuzivunja? Kwa hayo na yanayotokana na hayo ndiyo lengo la waraka huu.mungu
akubariki uanaposoma Neno Lake.
AMRI
ZA MUNGU NI ZIPI NANI NGAPI?
1. Usiwe
na miungu mingine ila mimi.KUTOKA 20:3
2. Usijifanyie
sanamu ya kuchonga,wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni,wala
kilicho chini duniani,wala kilich majini chini ya dunia.usivisujudie wala
kuvitumikia;kwa kuwa mimi ,BWANA Mungu
wako ni Mungu mwenye wivu;nawapatiliza wana maovu ya baba zao,hata kizazi cha
tatu na cha nne chawanichukiao,name nawarehemu maelfu elfu wanipendao na
kuzishika amri zangu.KUTOKA 20:4-6
3. Usilitaje
bure jina la BWANA,Mungu wako maana BWANA hata mhesabia kuwa hana hatia mtu
alitajae jina lake bure.KUTOKA 20:7
4. Ikumbuke
siku ya Sabato uitakase.Kwa siku sita utafanya kazi zako zote, lakini siku ya
saba ni Sabato kwa BWANA Mungu wako. Siku hiyo hutafanya kazi yo yote, wewe
wala mwana wako au binti yako, wala mtumishi wako wa kiume au wa kike wala
wanyama wako, wala mgeni aliye ndani ya malango yako.Kwa kuwa kwa siku sita, BWANA
aliumba mbingu na nchi, bahari na vyote vilivyomo ndani yake, lakini akapumzika
siku ya saba. Kwa hiyo BWANA akaibariki siku ya Sabato na kuifanya
takatifu.KUTUKA 20:8-11.Katika amri ya
nne,tunaagizwa kuitunza sabato.
SABATO
NI SIKU IPI?
Biblia inatuambia kuwa sabato ni siku ya saba katika
wiki.biblia inasema :-
“Baada ya siku ya sabato, maria Magdalena, salome na
maria mama yake yakobo walinunua manukato ili waupake mwili wa yesu .basi
alfajiri na mapema siku ya jumapili,walifika kaburini,jua lilipoanza
kuchomoza”.
MARKO 16:1-2(BIBLIA-HABARI NJEMA, KISWAHILI CHA
KISASA)
Hivyo hapo na habari ya ufufuko wa Yesu,tunaona kuwa
alifufuka jumapili amboyo ndiyo siku ya kwanza
ya juma soma MATHAYO 28:1
Ø Pia
biblia inatuonyesha siku ya kifo chake,ilikuwa ijumaa ambayo ndiyo maandalio ya
sabato.
“Siku hiyo ilikuwa
ijumaa,na maandalio ya siku ya sabato yalikuwa yanaanza .wale wanawake walioandamana na yesu kutoka Galilaya walimfuata Yosefu, wakaliona lile
kaburi na jinsi mwili wake Yesu ulivyowekwa .Halafu wakarudi
nyumbani,wakayatayarisha manukato na marashi ya kuupaka mwili wa Yesu .Siku ya
sabato walipumzika kama ilivyoamriwa na sheria”LUKA 23:54-56
(BIBLIA TOLEO LA HABARI
NJEMA KISWAHILI CHA KISASA)
Kwahiyo tunaona kuwa
sabato siyo ijumaa wala Jumapili bali ni Jumamosi
5. Waheshimu baba yako na mama yako, ili upate
kuishi siku nyingi katika nchi anayokupa
BWANA Mungu wako.KUTOKA 20:12
6. Usiue. KUTOKA 20:13
7. Usizini. KUTOKA 20:14
8. Usiibe. KUTOKA 20:15
9. Usitoe ushuhuda wa uongo dhidi
ya jirani yako. KUTOKA 20:16
10. Usiitamani nyumba ya jirani yako. Usimtamani mke
wa jirani yako, wala mtumishi wake wa kiume au wa kike, wala ng’ombe wake au
punda wake wala cho chote kile alicho nacho jirani yako. KUTOKA 20:3-17,
KUMBUKUMBU LA TORATI 5:7-21
Ø Amri
za Mungu ni za muhimu kwa Nyakati zote na vizazi vyote.Yesu anatoa agizo hili
juu ya umuhimu wa amri za Mungu:-
“……………………….lakini ukitaka kuingia katika uzima
zishike amri MATHAYO 19:17
“Msidhani kwamba nimekuja kuondoa Torati au Manabii,
sikuja kuondoa bali kutimiza.Kwa maana,amin, nawaambia, mpaka mbingu na dunia
zitakapopita, hakuna hata herufi moja ndogo wala nukta itakayopotea kwa namna
yo yote kutoka kwenye Torati mpaka kila kitu kiwe kimetimia. Kwa hiyo, ye yote
atakayevunja mojawapo ya amri ndogo kuliko zote ya amri hizi, naye
akawafundisha wengine kufanya hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika Ufalme wa
Mbinguni, lakini ye yote azitendaye na kuzifundisha hizi amri ataitwa mkuu
katika Ufalme ya Mbinguni.Kwa maana nawaambia, haki yenu isipozidi haki ya waandishi
wa sheria na Mafarisayo, kamwe hamtaingia katika Ufalme wa Mbinguni”.MATHAYO
5:17-19
Ø Watu
wengi leo ,hutoa udhuru wa kuzishika Amri kumi za Mungu,kwa madai ya kumwamini
na kumpenda Yesu.Husema “Ukimwamini Yesu tu,inatosha,hakuna haja ya kuzishika amri”.je,
udhuru huo Yesu aliukubali katika maandiko matakatifu?
Yesu mwenyewe alisema;-
“Mkizishika
amri Zangu mtakaa katika pendo Langu, kama Mimi nilivyozishika amri za Baba
Yangu na kukaa katika pendo Lake.”YOHANA 15:10
“Kama mnanipenda,
mtazishika amri Zangu.”YOHANA 14:15
“Kwa
kuwa huu ndio upendo wa Mungu, kwamba tuzitii amri Zake. Nazo amri Zake si
nzito”.1YOHANA 5:3
Ø Je
amri za Mungu kila mtu anapaswa kuzijua na kuzishika? Au kwa ajili ya watu
Fulani tu,au dhehebu Fulani tu?
Biblia Inasema:-
“Hii ndiyo ya maneno ;yote yamekwesha sikiwa,mche
mche Mungu, nawe uzishike amri zake maana kwa jumla ndiyo impasavyo mtu “MHUBIRI
12:13
Hivyo tunaona kuwa biblia inasema kuzishika amri za
mungu kunampasa kila mtu yeyote anayejifahamu kuwa yeye ni mtu ‘ anapaswa
kuzishika amri za mungu. Hata kama mtu angesema’Mima nampenda mungu’ au mimi
nimeokoka; kama bado hataki kuzishika Amri za mungu ;madai yake huyo hayaungwi
mkono na Biblia kwan maandiko yanasema”
Wokovu u mbali na wasio haki’ kwa maana hawajifunzi
amri zako ZABURI 119:115
‘’Umewakataa wote wazikosao amri zako ,kwa maana
hila zao ni uongo’’ZABURI 119:118
‘’Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye ikiwa
tunashika amri zake.Yeye asemaye nimemjua ,wala hazishiki amri zake,ni uongo wala
wala kweli haimo ndani yake’’YOHANA2:34.MITHALI28:9
Ø Kwa
hiyo hapana maandiko yatwambia kuwa,kutozitii amri za mungu nab ado huku
tukijiita wakristo,Watu wa mungu Wanaompenda Mungu ,Walio okoka, Washika ibada
na majina mengine kama hayo ya kujisifia uumini Huku tunapinga na kuvunja amri
za mungu Maandiko yanasema watu wa namna hiyo ni ‘’WAONGO’’NA tunajua kuwa
mwongo hawezi kwenda mbingni (soma ufunuo 21;8,22;15)Maana uongo bado ni
uvunjaji wa amri ya tisa (KUTOKA 20;16)Katika amri kumi za MUNGU
Wengi wamefundishwa kuzishika amri baadhi na zingine
kuziacha,na kutoa mafundisho kuwa eti hizi hazituhusu,maana ziliondolewa na
yesu pale msalabani n.k kwa mfano,amri ya pili inayokataza ibada ya sanamu
(KUTOKA 20:4-6)NA amri ya nne inayo waigiza watu waitunze sabato siku ya saba
ya juma (KUTOKA 20:8-11)amri hizi zimevunjwa wazi na kuondolewa na watu
mamilion wanafundishwa na viongozi wao wa makanisa kuwa amri hizo kwa sasa
haziwahusu.Huu ni mpango mkuu wa Yule adui (SHETANI)kuwafanya watu wamwasi
Mungu kwa kuzivunja amri zake.
BIBLIA
YENYEWE ANATOA ANGALIZO HILI:-
“Maana mtu awe yote atakaye shika sheria yote ila
akajikwaa katika neon moja amekosa juu ya yote kwa maana yeye
alisema,usizini,pia alisema usiue.Basi ijapokuwa hakuzini lakini umeua umekuwa
mvunja sheria. Semeni ninyi na kutenda kama watu watakao hukumiwa kwa sheria ya
uhuru’’YAKOBO 2:10-12, SOMA PIA, MATHAYO 5:19
Kwa nini watu
wengi wachague kuvunja amri za mungu na hali ya kuwa amri ziko wazi katika neon
lake –maandiko matakatifu.?
Biblia ainatoa sababu ya uvunjaj I wa sheria hizo za
mungu kauli ya yesu iliyo sema:-
Akawambia ,isaya alitabiri vema juu yenu ninyi
wanafiki kama ilivyo andikwa,watu hawa huniheshimu kwa midomo ,ila mioyo iko
mbali name:Nao waniabudu bure wakifundisha mafundisho yalio maagizo ya
wanadamu.
Ninyimwaiacha amri ya mungu na kuyasniks mapokeo ya
wanadamu .Akawaambia vema mwaikataa amri ya mungu mpate kuyashika mapokeo
yenu’’ MARKO 7:6-9
Ø Biblia
inatwambia sababu ya wengi kuvunja amri za mungu ni mapokeo ya
wazee(VIONGOZI)wengi leo wanafundishwa mapokeo ya wanadamu na kuyatii kwa
uaminifu kuliko amri za mungu ,hata kama mapokeo hayo hawayapatii ushindi wa
maandiko hutetea kwa msimamo mkali wa kulinda itikadi za madhehebu kwa hiyo
Miongozo,kanuni,katiba,desturi na heshima kwa viongozi wanadamu vimechukua
nafasi kuliko maandiko matakatifu yaliyo neon laMungu.
Ø Ndugu
msomaji mpaka haoa utakuwa umegundua umuhimu wa kuzijua na kuzitii amri kumi za
mungu amua kuishi kulingana na matakwa ya mungu katika amri zake. Kwani kuna
mbaraka mkubwa katika kuzishika amri maana Neno la MUNGU lasema,
“Aishikaye amri hatajua neon baya na moyo wa mwenye
hekima hujua wakati na hukumu MHUBIRI 8:5
Ø Tena
watu wa mungu waaminifu watatambuliwa tu kwa kuzishika amri za mungu na si
vinginevyo hivi ndivyo neon la Mungu linavyothibitisha kwa kusema
’’Na waende kwa sheria na ushuda ikiwa
hawasemi sawasawa na neon hili bila shaka kwa hao hapana asubuhi ASAYA 8:20
’’Hapa ndipo penye subira ya watakatifu hao
wazishikao amri za Mungu na imani ya Yesu’’UFUNUO 14:12
HITIMISHO
Katika kuzishika amri za Mungu ,mwanadamu anaweza kuishi kwanzo.Ndivyo
nenola mungu linavyosema ,
“Naye akanifundisha ,akaniambia ,moyo wako
uyahifadhi maneno yangu shika amri zangu ukaishi” MITHALI 4:4
“ Nikawapa amri zangu na kuwaonyesha hukumu zangu
ambazo mwanadamu ataishi kwazo. Kama akizitenda” EZEKIEL 20:11
“Naye akaandika juu ya mbao mfano ya maandiko ya
kwanza zile amri kumi alizo waambia bwana huko mlimani toka kati ya moto siku
ya mkutano ; Bwana akanipa”KUMBUKUMBU LA
TORATI 10:4
“Bali agano hili ndilo natakalo fanya na nyumba ya
Israeli,baada ya siku zile,asema Bwana;nitatia sheria yangu ndani yao na katika
mioyo yao nitaiandika;name nitakuwa Mungu wao,nao watakuwa watu wangu.”YEREMIA
31:33
“Mwanangu, shika maneno yangu na
kuyahifadhi maagizo yangu ndani yako.Shika maagizo yangu nawe utaishi, linda
mafundisho yangu kama mboni ya jicho lako. Yafunge katika vidole vyako,yaandike
katika kibao cha moyo wako.”MITHALI 7:1-3